SWAHILI
Hili ndilo neno kuu la Mkutano wa Injili wa hadhara ambao unafanyika viwanja vya Kanisa la Waadventista Wa-Sabato Ilala.
Mnenaji mkuu wa mkutano huu ni
Mwinjilisti Yared Omolo. Kama Bwana alivyomtumia hapo kabla, atamtumia
pia kwa majuma mawili tangu tarehe 18-31 Julai 2015.
Pia kutakuwa na masomo ya Afya yatakayotolewa na daktari kila siku ya mkutano.
Sambamba na hilo, kutakuwa na huduma ya upimaji wa afya za watu.
Karibu wewe, jirani, ndugu, jamaa na rafiki yako tubarikiwe sote kwa pamoja.
"KARIBU.. KARIBU.. KARIBU."
Sabato ya tarehe 20 Desemba 2014 ilikuwa ni siku maalum ya kumshukuru Mungu kwa wema na fadhili zake kwa mwaka 2014. Siku hii iliongozwa na Kwaya ya Kanisa ambao walimtukuza Mungu kwa nyimbo za sifa na shukrani tangu vipindi vya asubuhi mpaka jioni. Pia ilikuwa ni siku ambayo Kwaya ya Kanisa ilitambulisha rasmi albam yake iliyorekodiwa ndani ya mwaka huu 2014 iitwayo ''MTUKUZENI".
Kwaya ya Kanisa ikiimba wakati wa Ibada asubuhi
Ruth Chaulo akihudumu katika Shule ya Sabato na
Mwalimu Daniel Sempambo akiiimba pamoja na Kwaya.
Mwalimu Daniel Sempambo akiiimba pamoja na Kwaya.
Wanakwaya wakiimba wakati wa kipindi cha mchana.
Kwaya
hii ya kanisa la waadventista wasabato Ilala imepata kuhudumu katika
siku maalum ya kuweka wakfu kanisa la waadventista wasabato Kimara
terehe 23/11/2014 katika viwanja vya kanisa hilo.
Kwaya
hii imepata kutoa huduma ya uimbaji kama kwaya aliyoalikwa siku hii na
kuimba nyimbo kama;-"Mungu wetu twamshukuru sana" huu ukiwa ni wimbo
maalum,hivi nilivyo mimi,Yesu aliniita njoo na mwisho kwaya hii ikapata
kuimba wimbo wa pamoja na kwaya ya Kimara ambao unaitwa "Naweka hazina
yangu Mbinguni"
PICNIC YA VIJANA
Kiongozi wa Vijana(AY) Anthony Mwainyekule akitoa somo fupi kuhusu vijana.
Anthony Mwainyekule akiongoza vijana katika mazoezi ya viungo
Baadhi ya vijana wakifurahia ukuu wa Mungu kupitia mchanga wa bahari
.mslaba umekamilika sasa...
STAND UP FOR JESUS