Tigo
  • MTANZANIA AMCHUMBIA MWIMBAJI WA AMBASSADORS OF CHRIST YA RWANDA

     Mwimbaji wa Sauti ya kwanza wa Ambassadors of Christ ya Rwanda Humure Rebecca amechumbiwa na Mwimbaji na Kiongozi wa kundi la Voices of Victory la jijini Dar es salaam,Warren Bright,sherehe fupi ya uchumba ilifanyika nyumbani kwa wazazi wa Warren Bright,Kunduchi jijini Dar es salaam Agosti 17,2013 na ilihudhuriwa na baadhi ya waimbaji mbalimbali wa nyimbo za injili nchini Tanzania na mwimbaji wa kiume wa Ambassadors of Christ, Nelson Manzi.

     Warren ambaye ameweka picha za tukio hilo katika wasifu wake wa facebook amesema harusi yao inatarajiwa kufanyika hivi karibuni. Warren pia amekuwa mmoja wa waimbaji wa kwaya hiyo ya Ambassadors of Christ ambapo amekuwa akienda nchini Rwanda kuimba na kwaya hiyo pamoja na kufanya baadhi ya ziara pamoja na kwaya hiyo.


     
      Waimbaji wengine wa Ambassadors of Christ ambao wamefunga pingu za maisha na waimbaji wenzao ni Dushimimana Desire ambaye hivi karibuni alimuoa mwimbaji wa kwaya nyingine ya mjini Kigali na Umurisa Yvonne mwimbaji wa solo ya wimbo wa Kwetu Pazuri aliyeolewa na Josué Blaise Habimana aliyekuwa mwimbaji wa Halelujah Choir ya Gisenyi, Rwanda na kwa sasa wana mtoto mmoja wa kike.

    Warren wa pili kutoka kushoto akiimba pamoja na waimbaji wa Ambassadors walipotembelea nchini Kenya mapema mwaka huu. Habari kwa hisani ya networkedblogs, Picha zote mali ya Warren Bright. GK inawatakia kila la kheri
  • You might also like