Wakati mgogoro wa chama cha
wananchi CUF ukiendelea na huku ikielezwa moja ya chachu ya mgogoro huo
ni kutoka chama cha demokrasia CHADEMA, leo September 30 2016 Mwenyekiti
wa CHADEMA, Freeman Mbowe ammejibu tuhuma za kuwa CHADEMA imekuwa
wakala wa mgogoro kwenye chama cha CUF, Mbowe amesema…….
Prof
Lipumba ambaye mara kwa mara amesikika akisema kuwa CHADEMA ni
wachochezi wakubwa na wanapandikiza mgogoro ndani ya CUF, sikusudii
kumjadili Lipumba na nikiendelelea kumjadili nitampa nafasi aliyokuwa
nayo zamani’
Sisi
kama chama cha siasa tutaendelea kushirikiana na chama cha wananchi
CUF, tutaendelea kuheshimu maamuzi yanayofanyika kwenye vikao halali
vya chama cha wanachi CUF, tutaendelea kufanya kazi na wabunge na
madiwani wa UKAWA, tunaomba viongozi wote wa CHADEMA wapuuze na wasimpe
ushirikiano wowote Prof. Lipumba’;-Mbowe
